Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Kaizer Chiefs: Tunatakiwa kuwa bora ugenini

Hunt Pic Data Kocha Kaizer Chiefs: Tunatakiwa kuwa bora ugenini

Mon, 17 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Wakati Simba wakijipanga kulipiza kisasi Uwanja wa Mkapa, Dr es Salaam dhidi ya Kaizer Chiefs, kocha wa wapinzani wao, Given Hunt amesema hata kama wameshinda vizuri nyumbani lakini bado Simba ni timu ya kuchungwa wakiwa nyumbani.

Wakati Simba wakijipanga kulipiza kisasi Uwanja wa Mkapa, Dr es Salaam dhidi ya Kaizer Chiefs, kocha wa wapinzani wao, Given Hunt amesema hata kama wameshinda vizuri nyumbani lakini bado Simba ni timu ya kuchungwa wakiwa nyumbani. Hunt alisema bado kuna kazi nzito katika mchezo wa marudiano katika kuupanua ushindi wao au kuulinda ambapo wachezaji wake wanapaswa kuwa makini na mchezo ujao. “Sio nzuri ukiwa na furaha sana, tumemaliza dakika 45 za kwanza ili mechi imalizike tunatakiwa kuwa bora zaidi ugenini, Simba ni timu inayocheza vyema nyumbani,” alisema Hunt. “Hatutakiwi kuona tumemaliza mchezo tunakwenda kwenye mechi ngumu zaidi ambayo tunatakiwa kuwa na mpango mzuri wa kushindana nao.”

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz