Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiwanda cha risasi Kenya chajiendesha kwa hasara ya mamilioni

Bullet Pic Kenya Kiwanda cha risasi chajiendesha kwa hasara ya mamilioni

Mon, 1 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiwanda cha kuzalisha risasi cha nchini Kenya KOFC kimeshindwa kukidhi mahitaji ya soko la ndani na kupelekea hasara kubwa ya kifedha ya dola milioni 6.2 swa na shilingi bilioni 14.301 za kitanzania mwaka 2019.

Haya yamebainishwa na Mkaguzi Mkuu wa Serikali Nancy Gathungu wakati wa uwasilishaji wa ripoti ya ukaguzi wa mapato namatumizi kwa taasisi nchini humo.

Amesema kuwa kiwanda hicho kimepoteza jumla ya dola milioni 4.2 sawa na shilingi bilioni 9.7 za kitanzania kwa mwaka 2018.

Aidha uchunguzi huo ulibaini kuwa kiwanda hicho kilifanya jumla ya mauzo ya dola milioni 5.3 sawa na shilingi bilioni 12.22 za kitanzania wakati gharama za uzalishaji zikiwa juu kwa dola milioni 11.3 saa na shilingi milioni 26.04 hali iliyopelekea upotevu wa dola milioni 6.2 sawa na shilingi milioni 14.3 za kitanzania.

"Uongozi wa kiwanda hiki umeeleza kuwa sababu kuu iliyopelekea upotevu huu mkubwa fedha kuwa ni ubovu wa na uchakavu wa vitendea kazi ambao unafika asilimia 40 jambo ambalo limepelekea kushindwa kufikia mahitaji ya soko la ndani" amesema Gathungu wakati akiwasilisha ripoti hiyo.

Aidha Mkaguzi huyo amehoji juu ya ubovu wa vitendea kazi hivyo kwa kuubana uongozi huo kuhusu kutozingatia ukarabati wa vitendea kazi hivyo katika muda muafaka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live