Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#KirusiKIPYA: Rwanda yasitisha safari za ndege mataifa ya Kusini mwa Afrika

Press27 Scaled #KirusiKIPYA: Rwanda yasitisha safari za ndege za mataifa ya Kusini mwa Afrika

Mon, 29 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Rwanda imetangaza hatua mpya ambazo ni pamoja na kusimamisha safari za ndege kwenda na kutoka nchi za kusini mwa Afrika.



Abiria wote wanaowasili lazima wathibitishe kutokuwa na virusi vya corona na wafanyiwe vipimo vya marudio wanapowasili .

Karantini ya siku saba pia imerejeshwa kwa wasafiri wanaotoka nchi zilizoathiriwa hivi karibuni na mawimbi mapya.

Wale wote wanaohudhuria mikusanyiko kama vile harusi na mazishi lazima wapate chanjo kamili.

Kufuatia maagizo ya serikali kuhusu usafiri, shirika la ndege la Rwandair limesitisha huduma kwenda Afrika Kusini, Zimbabwe na Zambia:

Chanzo: www.tanzaniaweb.live