Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kibadeni awapa darasa Simba ikiivaa AS Vita

Kibadeni Pic Data Kibadeni awapa darasa Simba ikiivaa AS Vita

Tue, 30 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Wakati kocha wa AS Vita, Florent Ibenge akiamini wanaweza kupata matokeo ugenini dhidi ya Simba, Abdallah Kibadeni amesema mechi hiyo ni ngumu kwa Simba na wanapaswa kucheza kwa nidhamu ya hali ya juu.

Simba itacheza na AS Vita jijini Dar es Salaam, mechi ambayo wawakilishi hao wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika wanahitaji pointi moja ili kufuzu kucheza robo fainali.

Awali timu hiyo yenye pointi 10 iliifunga AS Vita kwao mechi ambayo Ibenge anasema Simba walikuwa bora zaidi kwenye mechi ya awali na ndicho kiliwasaidia kupata matokeo ugenini akiamini hata wao wanaweza kupindua meza Jumamosi.

Wakati Ibenge akitoa kauli hiyo, Kibadeni kocha wa zamani wa Simba ameipa angalizo timu yake hiyo akisisitiza kwamba mechi ya Jumamosi ni ngumu kwa Simba.

"Kikubwa ni Simba kuiheshimu AS Vita, pamoja na kwamba waliifunga mechi ya awali tena ikiwa nyumbani, lakini ni timu yenye uwezo na uzoefu wa kutosha kimataifa.

"Bila shaka watakuja nchini wakiwa na malengo ya kulipa kisasi, kitu cha Simba kujifunza ni je? kama waliweza kuifunga AS Vita kwao basi hata wapinzani wao watakuja na dhana hiyo.

"Wacheze kwa kuiheshimu na wapambane kweli kweli ili kupata matokeo katika mechi hiyo," amesema Kibadeni

Kama watashinda, Simba itafikisha pointi 13 na kuipa nafasi ya kufuzu kucheza robo fainali bila kujali matokeo ya mechi yao ya mwisho ya kundi A dhidi ya Al Ahly itakayochezwa nchini Misri.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz