Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya yanufaika na mapato ya usafirishaji Uganda

Export Kenya yanufaika na mapato ya usafirishaji Uganda

Fri, 24 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mapato ya Serikali ya Kenya yanayotokana na usafirishaji wa bidhaa nchini Uganda yanatajwa kuongeza kwa kasi kwa katika kipindi cha mwezi Aprili mwaka 2021, kutokana na kuondolewa kwa vizuizi vingi vya kibiashara vilivyokuwepo baina ya nchini hizo mbili.

Takwimu zilizokusanywa na kituo cha Takwimu cha Taifa nchini Kenya, zimeonesha kuwa kati ya mwezi Aprili hadi julai 2021 wameweza kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 25.97 ya Kenya sawa na bilioni 500 za Tanzania ambayo ni sawa na asilimia 56.64, kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa kwa takriban miaka mitatu iliyopita.

Hata hivyo ongezeko hilo limechochewa na hatua ya kuondolewa kwa vizuizi vya kibishara, mara baada ya makubaliano yaliyo fikiwa na Baraza la Umoja wa Afrika Mashariki kunuia kuwa kwa nchi wanachama kuondoa vizuizi hivyo ili kukuza uchumi wa eneo la Afrika mashariki.

Nchi hizi mbili zilikubaliana kuondosha vikwazo hivo kwa kupunguza mlima wa kodi uliokuwepo kati yao, ambapo Uganda imepunguza asilimia 13 za kodi kwa bidhaa za Kenya, huku ikipunguza asilimia 12 ya kodi iliyokuwa imewekwa katika usafirishaji wa dawa za kutibu.

Kenya wao wamekubali kuondoa asilimia 35 ya kodi iliyokuwa imewekwa katika usafirishaji wa mitungi ya gesi kutokanchini Uganda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live