Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya yaibana Rwanda kwao

32e79c261db4e9c42dee67ed009138b2 Kenya yaibana Rwanda kwao

Tue, 7 Sep 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

TIMU ya taifa ya Rwanda, Amavubi, imeshindwa kutumia vyema uwanja wa nyumbani wa Nyamirambo jijini hapa, baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Kenya katika mchezo wa hatua ya kwanza ya kufuzu kushiriki Kombe la Dunia Qatar 2022 uliochezwa juzi Jumapili.

Kenya walitangulia kufunga bao katika dakika ya tisa kupitia kwa naodha wake, Michel Olunga kabla ya wenyeji kusawazisha katika dakika ya 21 kwa bao la Abdul Rwatubyaye.

Katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo kulikua na utengenezaji mdogo wa nafasi za kufunga huku Harambee Stars muda mwingi wakimiliki mpira bila mashambulizi ya hatari na Amavubi wakicheza kwa kujilinda kwa muda mrefu.

Kikosi cha Amavubi chini ya Kocha Mkuu, Vincent Mashami kililazimika kufanya mabadiliko ya mapema dakika ya 29 kwa kumuingiza mshambuliaji anayechezea Simba ya Tanzania, Meddie Kagere badala ya Lague Byiringiro kuumia.

Kipindi cha pili kilianza kwa shambulizi la hatari kutoka kwa Harambee Stars pale Olunga alipopokea pasi ndefu akiwa ndani ya eneo la adui, lakini alishindwa kupiga shuti la nguvu kutokana na kukabwa vilivyo na mabeki wa Amavubi

Lakini katika kipindi hicho hicho, Amavubi walibadilika kimbinu na kuanza kufanya mashambulizi na dakika ya 65, Meddie Kagere alikosakosa kufunga baada ya kupokea mpira wa adhabu uliopigwa na naodha wa timu hiyo, Haruna Niyonzima.

Amavubi walifanya shambulizi jingine kupitia kwa Jacques Tuyisenge, lakini bidii za mlinda mlango wa Kenya zilionekena kwani alizuia mpira huo usiingie nyavuni.

Katika mzunguko huu wa kwanza kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2022, Rwanda ipo Kundi E pamoja na Mali, Uganda na Kenya. Kinara wa kundi hilo ndiye atakayefuzu kuingia hatua ya tatu na ya mwisho kwenye michuano hiyo.

Katika kundi hilo, Amavubi ndio inaoshikilia nafasi ya mwisho kwa ubora katika viwango vya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (Fifa) ikilinganishwa na timu zingine ilizopangwa nazo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz