Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya watamani unafuu wa bei ya mafuta Tanzania

Bei Ya Mafuta Kenya Yapanda Kenya watamani unafuu wa bei ya mafuta Tanzania

Fri, 22 Sep 2023 Chanzo: The Citizen

Kituo cha habari Cha CITIZEN nchini Kenya kimeeleza kuhusu wananchi wa nchi hiyo wanaoishi Karibu na mpaka wa Tanzania wakifurahia unafuu wa bei ya kununua mafuta wanayoipata baada ya kuvuka mpaka na kununua mafuta hayo nchini Tanzania huku wakishangaa inawezekanaje bei ya mafuta ipande Dunia nzima lakini Tanzania iwe nafuu.

Ni kama tunafaidi nchi ya Tanzania wakati sisi ni wakenya, kwa hivyo ningeuliza serikali yetu. Haya mafuta ya Tanzania kwani haya mafuta yanatoka wapi?.

Ikiwa mafuta imepanda Dunia nzima, kwanini mafuta ya Tanzania bei rahisi?….

“Tunapitia kwamba hali ya maisha imekuwa ngumu, maisha imekuwa juu. Petroli ndio hiyo imepanda na unajua petrol ndio kila kitu

Ile afueni tuko nayo kidogo sisi tuko karibu na mpaka, sisi tunaenda Tanzania tunakunywa mafuta japokuwa kuna wenzetu wako huku wanaumia sana kuna kiangazi pia… mambo ya mbole kwanza bwana Ruto angeacha mambo ya mbolea angetusaidia kwanza kutupunguzia mafuta ili gharama ya maisha kidogo iende chini.”

Chanzo: The Citizen