Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya kutumia akiba ya IMF kuilipa China

Imf Loasn Kenya Kenya kutumia akiba ya IMF kuilipa China

Wed, 22 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Kenya inafikiria kutumia akiba yake ya fedha kutoka Shirika la Fedha la kimataifa la IMF ili kuweza kulipa mkopo kutoka Serikali ya China baada ya Mfuko wa Hazina wa taifa nchini humo kutupilia mbali maombi ya kulipa deni hilo.

Taarifa iliyotolewa na uongozi wa Mfuko huo inasema kuwa inaweza kutumia mgao wake wa ziada wa akiba ya IMF ulio katika akaunti ya maalum ya Haki na mali (SDR) ambazo zinaweza kubadilishwa kuwa pesa za maendeleo ya serikali ili kuweza kuziba pengo hilo la bajeti ya nchini humo.

SDRs ni akaunti iliyo ndani ya IMF inayoruhusu kubadilisha fedha kutoka shilingi yoyote ile duniani kwa ajili ya kutatua changamoto za kiuchumi zinazoikumba nchi husika.

Hata hivyo Kenya ilitarajia kuongeza muda zaidi wa kufanya malipo hayo kutoka kwa wakopeshaji wa pande mbili ikiwemo China kuanzia mwezi Januari 2021 kwa kufanya malipo kwa awamu ya miezi sita huku ikijipanga kuilipa China bilioni 50 katika vipindi vyote viwili.

Jambo ambalo halikupokelewa vyema na wakopeshaji wakubwa wa China ikiwemo benki ya Exim, kwani wamedai hatua hiyo ina kwamisha shuughuli zingine za maendeleo zinazo dhaminiwa na Serikali ya China.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live