Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya kuanzisha safari visiwa vya Caribbean

Kq Kenya kuanzisha safari visiwa vya Caribbean

Thu, 7 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Kenya inapanga kuanzisha ushirikiano mpya wa safari za anga baina yake na nchi za visiwa vya Caribbean ili kuweza kuunganisha biashara za Mjii Mkuu wa Nairobi katika soka la kimataifa utakaosaidia kupambana na mtikisiko mkubwa wa uchumi uliosababishwa na athari za Corona.

Kenya imeandika mkataba unaohusu ushirikiano huo, utunzaji wa mazingira, kukuza biashara na kuongeza uwekezaji wakati wa ziara ya Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje Visiwani humo.

Mkataba huo umegusia makubaliano ya huduma za anga kwa nchi hizo mbili, huku hatua ya kwanza katika makubaliano ikiwa ni kuyaruhusu mashirika ya ndege ya pande zote mbili kukubaliana na kushirikiana katika safari hizo.

Makubaliano hayo yamesainiwa na Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje nchini Kenya, Raychelle Omamo, na kueleza kuwa nchi hizo hazikuwahi kuwa na uhusiano wa moja kwa moja wa usafiri wa anga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live