Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya kuanza kuwaunganisha huduma ya Internet watumiaji umeme vijijini

AARpBrZ Kenya kuanza kuwaunganisha huduma ya Internet watumiaji umeme vijijini

Fri, 3 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kampuni ya Umeme ya Kenya Power baada ya kutajwa kuingiza hasara kwa muda mrefu sasa imekuja na mbinu ya kuunganisha huduma ya internet kwa mamilioni ya wateja wake kama sehemu ya mpango mpya kuongeza matumizi ya data ya simu nchini humo na kukuza vyanzo vipya vya mapato.

Hii ni hatua iliyochukuliwa na KPLC ambao wamekuwa wakikodisha nyaya za fibre-optic zilizounganishwa kwenye laini zake za usambazaji kwa watoa huduma za mtandao.

Kenya Power imesema sasa itawalenga moja kwa moja na kuwaunganisha wateja wa vijijini wakati wa kuongeza watumiaji wa umeme na kupenya nchini kote kwa kuunganisha mamilioni ya nyumba mpya katika maeneo ya vijijini kwenye gridi ya taifa.

Mwaka 2010, Kenya Power ilitia saini mkataba wa miaka 10 na kampuni ya SafariCom kukodisha miundombinu yake ya nguzo na nyaya wenye thamani ya zaidi ya Tsh. Bilioni 8.

Pia ilitia saini mikataba na makampuni ya mawasiliano ya simu ya Wananchi Group na Jamii Telecommunications huku kila moja ikisaini mikataba ya miaka mitano yenye thamani ya Tsh. Bilioni 7.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live