Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya: Waandamanaji wanakabiliwa na ukatili wa polisi

Maandamano Kenya Ghsz Kenya: Waandamanaji wanakabiliwa na ukatili wa polisi

Tue, 23 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vifo vya makumi ya watu nchini Kenya kufuatia wimbi la maandamano huku polisi wakikabiliana na maandamano hayo, vilianza na mauji ya kupigwa risasi Rex Masai mwenye umri wa miaka 30.

Mauaji hayo yamezidi kuondoa imani ndogo iliyokuwepo kuhusu jukumu la polisi la kudumisha utulivu. Huku msururu mpya wa maandamano ukikaribia kuanza, kuna wasiwasi jinsi vikosi vya usalama vinavyoshughulikia maandamano hayo.

Tarehe 20 Juni ilikuwa siku ya pili ya maandamano dhidi ya mswada wa fedha ambao ungeongeza kodi mpya. Siku iliyotangulia haikuwa na matukio makubwa, lakini jua lilipotua siku ya Alhamisi, kila kitu kilibadilika katikati ya mji mkuu, Nairobi.

Waandamanaji walizidi kufanya maandamano. Maafisa wa polisi waliacha kutumia maji ya kuwasha na gesi ya kutoa machozi na kufyatua risasi za moto.

Masai alijikuta katikati ya vurugu hizo. Alipigwa risasi ya paja na kuvuja damu hadi kufa. "Damu yake ilitapakaa mikononi mwangu," anasema rafiki yake, Ian Njuguna, ambaye alimkimbilia kujaribu kumsaidia alipoanguka chini.

Wakati yeye na rafiki mwingine wakijaribu kumbeba kwenda nae hospitali ya karibu, anasema, “afisa alitupiga mabomu ya machozi [tulipokuwa] tumembeba rafiki yetu aliyekuwa anakaribia kufa." "Tulikuwa tukizungumza naye kwa majonzi, tukimsihi asituache."

Takribani maafisa wanne wa polisi kufikia sasa wanakabiliwa na mashtaka ya kuwapiga risasi na kuwaua waandamanaji katika kipindi cha wiki nne zilizopita, huku kukiwa na miito ya kutaka haki itendeke kwa waathiriwa wa matumizi ya nguvu kupita kiasi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live