Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya Airways yaweka pungiza la 30% ya tiketi za ndege

Discountw Shirika la ndege Kenya la toa punguzo la 30% tiketi za ndege

Wed, 22 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la ndege la Kenya, limetangaza punguzo la bei za tiketi hadi asilimia 30 kufuatia kuporomoka kwa mapato katika shirika hilo hali iliyosababishwa na mlipuko wa ugonjwa wa Corona.

Punguzo hilo la bei limefanywa huku likijumuisha maeneo yote ambako ndege hizo zinatua ispokuwa kwa safari za Guangzhou , China, Dar es Salaam, Tanzania, Juba, pamoja na Dubai sambamba na safari za ndani zinazoelekea Mjii Mkuu wa Nairobi pamoja na safari zote zinazo anzia Johannesburg kuelekea Dubai.

Punguzo hilo linawalenga wateja wote watakao kata tiketi kabla ya sepyemba 24 , 2021 hadi March 31,2022.

"Sisi kama Shirikia tumeweka umakini zaidi katika kumjali mteja ili kufanikisha shughuli zetu endelevu za kibiashara kwa kuwapa wateja wetu ofa kama hizi za kusisimua ambazo zinakidhi mahitaji yao katika wakati huu" Amesema Afisa Mkuu wa Biashara wa shirika hilo.

Pungozo hili la bei limekuja wakati Sekta ya usafiri wa anaga nchini humo ikiwa inapambana kujiokoa kutoka kwenye mporomoko mkali wa uchumi kufuatia janga la Corona.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live