Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya Airways yashutumiwa kuendesha shirika kwa ukiritimba

Kq Dreamliner KQ na washirika wake washutumiwa kwa ukiritimba

Thu, 28 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la ndege la Kenya KQ sambamba na washirika wake wameshutumiwa na Shirika la udhibiti barani Afrika kwa kuendesha shughuli zao za kibiashara katika mfumo wa ukiritimba.

KQ na washirika wake ambao ni Precision Air ya Tanzania, Europe Air France na KLM waliingia makubaliano ya kibiashara ambayo hayajaweka bayana mchanganuo wa bei za tiketi katika njia ambazo ndege hizo zinapita.

"Ushirika huu wa kibiashara umekuza masoko ya pande zote kikanda na kimataifa lakini hakuna ushindani wa kutosha kwenye bei za kuuza tiketi na hii si sawa, hivyo ni sawa kusema kuwa wanendesha shughuli zao kwa mfumo wa ukiritimba" imesema ripoti hiyo.

Utafiti huo ulifanywa kwa ajili ya kupata muelekeo wa sekta ya usafiri wa anga Afrika kwa kutambua ukuaji wa masoko, ushindani pamoja na uendeshwaji wa Mamlaka za usafiri huo kwa mataifa 24 yanayoshiriki katika tafiti hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live