Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kauli ya mwimbaji Size 8 baada ya kupoteza ujauzito

A13611e210f1f9f0 Kauli ya mwimbaji Size 8 baada ya kupoteza ujauzito

Fri, 1 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Size 8 na mumewe DJ Mo wameelezea kilichosababisha kuharibika kwa mimba ya mwanamuziki huyoHii ni mara ya pili kwa wanandoa hao kumpoteza mtoto kabla ya siku za kuzaliwa kutimiaDJ Mo akiwa mwingi wa majonzi, alisema madaktari walifanya kila wawezalo kuyaokoa maisha ya kitoto hicho lakini haikuwezakana Hata hivyo, Size 8 alimshukuru Mungu kwa kumpa fursa nyingine ya kuishiWanandoa Size 8 na mumewe DJ Mo wametangaza kupitia kurasa zao za mtandao wa You Tube kwamba wamempoteza mtoto wao aliyekuwa tumboni kutokana na shinikizo la damu kwa mamake.

DJ Mo alisema alikuwa ziarani alipopigiwa simu kwamba mkewe Size 8 ambaye alikuwa mjamzito, alikuwa amelemewa na kukimbizwa hospitalini akiwa katika hali mbaya.

" Presha imekuwa juu sana tangu nilipopata ujauzito, kwa wakati mwingine tulilazimika kubadilia dawa ninazotumia ili kujaribu kuidhibiti,"Size 8 alisema.

Madaktari walilazimika kumfanyia mwanamuziki huyo upasuaji ili kuyaokoa maisha yake huku DJ Mo akiwa kando yake akijaribu kumchangamsha na kumpa tumaini.

Size 8 alisikika akiimba wimbo wa 'Yes Jesus loves me' wakati alipokuwa akifanyiwa upasuaji kwenye thieta.

" Hii sio kitu rahisi, nimekuwa hapa kwa zaidi ya mara tatu, ni vema kusimama na mke wako katika kila hali," DJ Mo alisema.

Hii ni mara ya pili DJ Mo na mkewe Size 8 kumpoteza mtoto kama bado hajafikia muda wa kuzaliwa, wa kwanza ilikuwa mwaka wa 2018 akiwa tayari amejifungua Ladasha Wambui ambaye ni mtoto wao wa kwanza.

Size 8 alimshukuru Mungu kwa kumpa tena fursa ya kuishi ingawa alikuwa amempoteza mwanawe.

" Kila kitu huja na wakati wake na hutendeka kwa sababu, ilikuwa tuyaokoe maisha ya mama, " Alisema DJ Mo.

Kwa pamoja DJ Mo na Size 8 wamejaliwa watoto wawili, wa kike na wa kiume.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke