Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni ya umeme Kenya kuhakiki wafanyakazi wake

KENYAPOWERS Kampuni ya umeme Kenya kuhakiki wafanyakazi wake

Fri, 19 Nov 2021 Chanzo: BBC

Wafanyakazi wote wa kampuni ya umeme nchini Kenya kukaguliwa.

Hatua hii inakuja baada ya madai ya rushwa dhidi ya baadhi ya wafanyakazi.

Hivyo wafanyakazi wa kampuni ya umeme 'Kenya Power' wanapaswa kukabidhi kadi zao za benki na taarifa za akaunti zao za fedha za simu ifikapo Jumatatu.

Mali zote zinazomilikiwa na wafanyakazi pamoja na wenzi wao pia zitachunguzwa.

Kampuni imeanzisha msako huo baada ya taarifa kuvuja mtandaoni kuwa wafanyakazi huwa wanauza umeme kwa wateja kwa njia isiyo halali.

Kenya Power iko katika mchakato wa kuiboresha huduma za umeme na kupunguza gharama za huduma hiyo.

Chanzo: BBC