Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagere ashindwa kuibeba Rwanda

Bc38d7241c7eccf72fcfe8a94589e93c.jpeg Kagere ashindwa kuibeba Rwanda

Thu, 1 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

NYOTA wa Simba, Meddie Kagere ameshindwa kuisaidia timu yake kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2022) baada ya timu hiyo kutoka suluhu dhidi ya Cameroon katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Japoma.

Rwanda yenye pointi sita, ilitakiwa kuifunga Cameroon, huku ikiombea Msumbiji iifunge Cape Verde iliyokuwa na pointi saba,, hivyo Rwanda kama wangeshinda wangefikisha pointi tisa.

Kagere pamoja na kuanza katika mchezo huo, lakini hakuwa tishio na hadi mwisho wa mchezo timu hizo zilitoka suluhu na kugawana pointi moja moja.

Ushindi wa Cape Verde wa bao 1-0 dhidi ya Msumbiji moja kwa moja umeifungisha virago Rwanda kwani imebaki na pointi zake sita, huku Cape Verde wakimaliza katika nafasi ya pili kwa pointi 10 na Cameroon vinara kwa pointi 11.

Amavubi kama ingefuzu ingekuwa ni mara yake ya pili kufanya hivyo tangu mwaka 2015 ilipocheza kwa mara ya kwanza fainali hizo katika soka

Timu mbili za kwanza kutoka katika kila kundi ndizo zinafuzu kwa fainali hizo, ambazo zitashirikisha timu 24 nchini Cameroon mwakani.

Chanzo: www.habarileo.co.tz