Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KCB YAILAZA GOR MAHIA KASARANI

Fbedd620060f58f16cdf29e1017ee735 KCB YAILAZA GOR MAHIA KASARANI

Wed, 10 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

NAIROBI, Kenya MABINGWA watetezi Gor Mahia imepata pigo jingine katika mbio zao za kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Kenya (FKFPL) baada ya kupoteza kwa mabao 2-0 kutoka kwa KCB kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Michezo wa Moi, Kasarani, jijini hapa.

Mchezaji aliyeingia katika kipindi cha pili akitokea benchi, David Simiyu na Victor Omondi walifunga mabao na kuongeza presha zaidi kwa mabingwa hao mara 19 wa Kenya.

Ushindi huo ambao ni wa kwanza kwa KCB baada ya kupoteza mechi zao tatu zilizopita, ulishuhudia timu hiyo ikipanda hadi katika nafasi ya pili ikiwa na poiti 29, sita nyuma ya vinara Tusker, wakati Gor imeporomoka hadi katika nafasi ya 13 wakiwa na pointi 16.

KCB imecheza mechi 14, Gor imecheza mechi 12.

KCB ilifanya shambulizi katika dakika ya pili kupitia kwa mshambuliaji wake, Henry Onyango ambaye alipiga kichwa akiunganisha mpira wa adhabu kutoka upande wa kulia, lakini juhudi zake zilizimwa na kipa wa Gor Mahia Oluoch.

Nafasi ya wazi ya Gor ilikuwa katika dakika ya 10 wakati Samuel Onyango alipomimina krosi ambayo ilitua kwa Mbrazil Wilson Silva, lakini iliingiliwa na kiungo mkongwe Michael Mutinda.

Dakika mbili baadae, KCB walikuwa na bahati ya kupata bao baada ya Kenneth Muguna ambaye alikuwa hajakabwa kupiga mpira wa kichwa ndani ya boksi lakini hakulenga lango.

Derrick Otanga aliikosesha nafasi ya wazi KCB kupata uongozi wa mchezo katika dakika ya 42 wakati alipopiga shuti lililomlenga kipa Oluoch baada ya Simon Munala kupiga krosi kutoka upande wa kulia.

Kocha wa Gor, Vaz Pinto alifanya mabadiliko mawili kwa pamoja, akiwaingiza Clifton Miheso na Abdul Karim wakichukua nafasi ya John Macharia na Alpha Onyango.

Katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya Kenya, Kakamega Homeboyz ilimaliza ukame wa ushindi mara tatu mfululizo baada ya kuwachapa mabingwa wa zamani Mathare United 2-1 katika Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka la Kenya kwenye Uwanja wa Moi juzi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz