Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jose Chameleone na mkewe wakiadhimisha miaka 13 ya ndoa

5cd9d5970ebb835c Jose Chameleone na mkewe wakiadhimisha miaka 13 ya ndoa

Wed, 9 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Mwanamuziki maarufu Jose Chameleon na mkewe Daniella Atim walikuwa wakionyesha penzi lao hadharani mitandaoni mwongo mmoja uliopita

- Hata hivyo, penzi lao linaonekana lilididimia baada ya Daniell kuhamia nchini Marekani ambapo amekuwa akiishi kwa miaka kadhaa sasa

- Inasemekana kwamba Chameleone anamchumbia mwanamke mwingine kwa sasa ndiposa ndoa yake inayumba

Mwanamuziki maarufu kutoka Uganda Jose Chameleone ameadhimisha miaka 13 ya ndoa na mkewe Daniella Atim.

Chameleone alisema anamheshimu mama wa watoto wake watano na atafanya kila awezalo kuhakikisha kwamba wanawe wanakuwa na maisha bora.

" Nakuthathmini sana, nakuombea maisha marefu, mama wa watoto wangu," Chameleone alisema.

Daniella na watoto wake walihamia nchini Marekani miaka kadhaa iliyopita ambapo alijifungua mtoto wake kitinda mimba.

Duru zinaarifu kwamba ndoa ya wawili hao imeingia doa na wameamua kusaidiana kulea watoto wao, aidha kuna fununu kwamba Chameleone anamchumbia mwanamke mwingine.

" Mama Abba, ningependa kuelezea furaha yangu kwako, umesimama nami hata kwa wakati mgumu, umekuwa rafiki wa dhati na kwa yote utasalia kuwa mama wa watoto wangu. Leo ikiwa ni siku ya kuadhimisha miaka 13 ya ndoa yetu ningependa kushukuru Mola kwa kila kitu," Chameleone alisema.

" Maneno pekee hayawezi elezea furaha yangu lakini namshukuru Mungu kwa kukuleta maishani mwangu, hebu na Mungu azidi kukulinda na kukuelekeza katika njia zifaazo.Furahia siku ya uadhimisho wa miaka 13 wa ndoa yetu," Aliongezea Chameleone.

Aidha, Chameleone alitupilia mbali madai kwamba ana mwanamke mwingie na kudai kwamba anampenda mkewe na kumshukuru kwa kumzalia watoto wa kupendeza.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke