Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Joe Cole na Ben Uzoh watisha Basketbal Africa League

JOE COLE Joe Cole na Ben Uzoh watisha Basketbal Africa League

Mon, 17 May 2021 Chanzo: eatv.tv

Mwanamuziki wa miondoko ya RAP wa nchini Marekani, Joe Cole na mchezaji kikapu wa zamani wa NBA, Ben Uzoh wameendelea kunogesha mashindano ya mpira wa kikapu ya Basketbal Africa League (BAL) baada ya michezo hiyo kuanza usiku wa jana nchini Rwanda.

Submitted by George David on Jumatatu , 17th Mei , 2021 Msanii wa RAP wa Marekani na mcheza kikapu wa timu ya Patriots Basketbal Club, Joe Cole akiichezea timu yake hiyo kwenye mchezo wa usiku wa jana.

Joe Cole anayeichezea timu ya Patriots Basketbal Club ya nchini Rwanda, ameisaidia timu yake hiyo kuibuka na ushindi wa alama 83 kwa 60 dhidi ya timu ya River Hoopers ya Nigeria anayeichezea nyota wa zamani wa NBA, Ben Uzoh.

Cole aliibuka na alama 17, rebaundi 1 na assisti moja wakati Ben Uzoh alipata alama 25, rebaundi 2 na assisti 3 lakini hazikutosha kuipa timu yake ushindi mbele ya wakali hao wa Rwanda.

Uzoh ambaye aliwahi kukipiga kwenye timu za New Jersey Nets, Clevelend Cavaliers na Toronto Raptors kwenye ligi kuu ya kikapu nchiniMarekani ‘NBA’ miaka ya 2010 hadi 2012 ameweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee aliyecheza NBA na kushiriki mashindano hayo.

(Ben Uzoh wa timu ya Rivers Hoopers ya Nigeria (katikati) akijaribu kuwatoka walinzi wa Patriots BC.)

Wawili hao wameendelea kuwa vivutio kwa wafuatiliaji wa mashindano hayo kwani ni dhahiri wamekuwa na umaarufu mkubwa uliowapa mashabiki wengi hususani kwa rapa Joe Cole ambaye nyimbo zake tele zilifanya vizuri Duniani ukiwemo ‘Can’t get it enough’.

Michezo itakayoendelea leo Mei 17, 2021 ni kati ya AS Douanes ya Senegal ambao watacheza dhidi Petroliers ya Angola saa 9:00 Alasiri, Zamaleki ya Misri nayo itapepetana na Ferroviario Maputo ya Msumbiji saa 12:30 jioni.

US Monastir ya Tunisia itakipiga dhidi ya GNBC kutoka Madagascar saa 4:00 usiku, wakati siku ya kesho Mei 18, 2021 Petro de Luanda ya Angola itaoneshana ubabe dhidi ya AS Police ya Mali, nayo AS Sale ya Morocco watakipiga dhidi ya FAP ya Cameroon.

Michuano hiyo itafikia tamati Mei 19, ambapo GNBC itakabiliana na Patriots,Maputo watamenyanja na AS Douanes nayo Zamaleki itacheza dhidi ya GSP.  

Chanzo: eatv.tv