Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hazina yaipiga chini M-Akiba Kenya

Phoness Hazina yaipiga chini M-Akiba Kenya

Mon, 11 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfuko wa Hazina wa Kenya umesitisha mpango wa utoaji wa dhamana ya fedha za matumizi ya simu kwa Taasisi za Serikali unaojulikana kama M-Akiba ya Benki Kuu kutoka kutoka kwa Nairobi Securities Exchange NSE na Central Depository and Settlement Corporation CD& SC kufuatia kuzorota kwa huduma hiyo.

Hatua hii imefikiwa mara baada ya kushindwa kwa dhamana ya kwanza iliyotolewa nje ya muda, uelewa mdogo wa aina ya bidhaa inayowekwa sokoni pamoja na huduma mbovu kwa wateja jambo lililopelekea kushuka kwa idadi ya usajili wa wateja wapya.

Hata hivyo inaelezwa kuwa mabadiliko ya sera yaliyofikiwa siku za hivi karibuni yanatajwa kuja kuchochea utendaji kazi katika sekta inayoshughulikia masuala ya utoaji wa mikopo wezeshi kwa Taasisi hizo.

Kitengo hicho kilizinduliwa mwezi Juni mwaka 2017 ili kuimarisha uhusiano uliopo kati ya soko la dhamana na maboresho ya ujumuishaji wa kifedha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live