Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Guinea-Bissau, Mauritania,  Ethiopia zafuzu Afcon

8bf558a6f400285ac6faba7cdfd0f72a.png Guinea-Bissau, Mauritania,  Ethiopia zafuzu Afcon

Thu, 1 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

GUINEA -Bissau, Mauritania na Ethiopua zimejihakikishia nafasi zao katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, Afcon 2022, zitakazofanyika Cameroon baada ya kukamilisha raundi ya mwisho ya michezo ya kufuzu kwa fainali hizo.

Guinea-Bissau imefuzu kwa mara ya tatu mfululizo shukrani kwa ushindi wao wa mabao 3-0 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika mchezo uliofanyika Bissau kwenye uwanja wa Septemba 24.

Piqueti alifunga bao la kwanza kwa Guinea-Bissau katika muda wa majeruhi wa kipindi cha kwanza. Congo ilijua kuwa ushindi pekee ndio utakaoiwezesha timu hiyo kufuzu kwa fainali hizo za Afcon, lakini matumaini yao yalifutwa wakati Alexandre Mendy alipofunga bao la pili katika dakika ya 73.

Jorginho aliiongezea ushindi Guinea-Bissau baada ya kufunga bao la tatu katika dakika ya 80.

Wakati huohuo, Mauritania iliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa Kundi E dhid ya Jamhuri ya Afrika ya Kati uliofanyika Banjul, ikiwa na maana kuwa Burundi hawawezi kuwakamata baada ya kufungwa 1-0 dhidi ya Morocco katika mchezo uliofanyika juzi.

Wakati suluhu kati ya Madagascar na Niger zimeinufaisha Ethiopia katika Kundi K, licha ya kuchapwa mabao 3-1 dhidi ya Ivory Coast wakati mchezo huo ukifutwa katika dakika ya 80 baada ya mwamuzi Charles Bulu kuanguka uwanjani.

Bulu alichezesha mchezo huo akichukua nafasi ya mwamuzi aliyepangiwa awali mchezo huo, ambaye hakuwasili hadi mchezo huo unaanza, na baadae mchezo huo ulifutwa.

Licha ya Madagascar kushindwa kuifunga Niger iliyopo mkiani katika kundi lao hiyo ikiwa na maana kuwa Ethiopia itashiriki kwa mara ya kwanza fainali hizo za Afrika tangu ilipofanya hivyo kwa mara ya mwisho mwaka 2013.

Kwingineko, mabao kutoka kwa Victor Osimhen, Oghenekaro Etebo na Paul Onuachu yaliisaidia Nigeria kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Lesotho.

Na katika Kundi I, bao la kusawazisha la dakika za mwisho kwa Senegal liliwafanya Eswatini kushindwa kupata ushindi wa kwanza katika kampeni zao hizo, baada ya mchezo huo kumalizika kwa sare ya 1-1.

Katika mchezo mwingine, Cape Verde walijihakikishia tiketi pekee iliyobaki ya kufuzu katika Kundi F kwa ajili ya fainali hizo za mwakani baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Msumbiji katika mchezo uliofanyika juzi kwenye Uwanja wa Estadio Nacional de Zimpeto.

Bao hilo pekee lilifungwa na Abdul Bangal katika dakika ya 58 na lilikuwa muhimu kwa wageni hao wanaojulikana pia kama Papa wa Bluu.

Cape Verde walimaliza katika nafasi ya pili wakiwa na pointi 10, kabla Rwanda (wenye pointi sita) na Msumbiji (4). Cameroon wameendelea kuwa katika nafasi ya kwanza wakiwa na pointi zao 11.

Nayo Nigeria ilimaliza mechi zake za kufuzu bila ya kufungwa baada ya juzi kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Lesotho katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Teslim Balogun jijini Lagos, Nigeria Jumanne.

Victor Osimhen ndiye alikuwa chachu ya ushindi kwa Nigeria au Super Eagles, baada ya kufunga bao moja na kusaidia jingine wakati Nigeria wakimaliza na pointi 14, wakiwa wa kwanza katika Kundi L.

Chanzo: www.habarileo.co.tz