Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gor Mahia yawatafuna mashemeji wao AFC kupitia penalti na kushinda KSh2M

Ea76eb93a6f81db9 Gor Mahia yawatafuna mashemeji wao AFC kupitia penalti na kushinda KSh2M

Mon, 5 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Mchuano wa mwaka huu wa fainali za Kombe la Betway ulikuwa kati ya mahasidi wa jadi AFC Leopards na Gor Mahia Mechi hiyo iliyoandaliwa katika uwanja wa Nyayo ilishuhudia K'Ogalo wakiibuka washindi kupitia matuta ya penaltiKulikuwa na mengi ya kupiganiwa wakati wa mchezo huo huku washindi wakihakikishiwa nafasi kwenye Kombe la Mashirikisho la Afrika Ushindi wa Gor pia una maana kuwa watatia kibindoni KSh 2 milioni kama zawadi ya kushinda kombe nyumbani

Miamba wa Ligi Kuu ya Kenya Gor Mahia ndio watawakilisha taifa wakati wa mchuano wa msimu huu wa Kombe la Mashirikisho la Afrika.

Gor walijitengea nafasi hiyo ya kipekee katika mtanange huo baada ya kuwapiga mahasidi wao wa jadi AFC Leopards 4-1 kupitia matuta ya penalti uwanjani Nyayo mnamo Jumapili, Julai 4 wakati wa fainali ya Kombe la Betway.

Kulikuwa na mengi ya kupiganiwa wakati wa mchezo huo huku washindi wakitia kibindoni KSh 2 milioni kama zawadi ya kushinda kombe nyumbani.

Kutokana na kiwango hicho cha pesa, timu zote zilianza mechi hiyo kwa haima ya juu wakiwa na motisha ya kutinga mabao mapema.

Hata hivyo, mechi hiyo iliamuliwa kupitia matuta ya penalti baada ya timu zote kushindwa kufunga bao wakati wa muda wa kawaida.

Ingwe, waliingia katika mechi hiyo wakiwa wamesukwa upya kuliko wapinzani wao na walikuwa na nafasi za wazi kufunga bao kunako dakika ya tano ya mchezo kupitia kwa Elvis Rupia lakini sogora huyo alipoteza.

Fowdi huyo nyota alikaribia kufunga tena punde baada ya muda wa mapumziko lakini alipoteza tena fursa hiyo.

Karim Abdul Nikiema alikaribia kuweka Gor Mahia kifua mbele dakika moja baadaye lakini mlinda lango wa Ingwe alipangua kombora lake.

Timu zote zilishindwa kufunga bao baada ya dakika 90 na hivyo mechi hiyo kulazimika kuamuliwa na mikiki ya penalti.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 073248269.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke