Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Google kuwekeza shilingi trilioni 2.3 Afrika

Googlepicdd Google kuwekeza Sh2.3 trilioni Afrika

Thu, 7 Oct 2021 Chanzo: mwananchidigital

Ili kuongeza kasi ya usambazaji wa intaneti barani afrika, kampuni ya Google imetangaza kuwekeza dola bilioni moja za Marekani (zaidi ya Sh2.3 trilioni) kwa miaka mitano ijayo.

Uwekezaji huo unakusudia kupunguza gharama hali itakayoongeza ari ya ujasiriamali wa kidijitali.

Taarifa ya Benki ya Dunia inaonyesha upatikanaji wa intaneti barani humu bado ni mdogo kwani ni chini ya theluthi moja ya watu wote zaidi ya bilioni 1.3 ndio wanatumia huduma hiyo.

Hata hivyo, bosi wa Google, Sundar Pichai amesema kuna mabadiliko yanaendelea siku za hivi karibuni ambazo “zitasaidia kuifanya iwe nafuu, itakayomnufaisha kila mmoja.”

Pichai anasema idadi kubwa ya watu Afrika wana chini ya miaka 18 hivyo kuwa fursa kwa siku zijazo.

Taarifa ya kampuni hiyo imesema uwekezaji huo unatarajiwa kuhamasisha ubunifu wa kidijitali kwa kuhakikisha watu wanapata intaneti ya uhakika kuwawezesha kubuni na kujaribisha miradi yao wakati wote, mahali popote.

Kati ya yatakayofanywa na fedha hizo ni kujenga miundombinu ya chini ya bahari itakayoiunanisha Afrika Kusini, Namibia, Nigeria na visiwa vya Mtakatifu (St) Helena na Bara la Ulaya.

Ahadi hiyo ni mwendelezo wa ile iliyotolewa na Google miaka minne iliyopita kwamba itatoa mafunzo kwa zaidi ya Waafrika milioni 10 waliopo kwenye sekta ya kilimo na kuwanoa katika Tehama.

Chanzo: mwananchidigital