Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Genge lawauwa wanawake na watoto Papua New Guinea – ripoti

Msitu Magamba Magamba Genge lawauwa wanawake na watoto Papua New Guinea – ripoti

Fri, 26 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makumi ya wanakijiji wameripotiwa kuuawa baada ya genge la vijana kufanya mashambulizi katika eneo la mbali la Papua New Guinea.

Walionusurika katika mauaji hayo wameelezea kusikia vilio vya majirani zao vya maumivu, na kuwatazama wengine wakichomwa mikuki walipokuwa wakijaribu kulikimbia genge hilo kwa mitumbwi.

Takriban watu 26 - ikiwa ni pamoja na watoto 16 - wameuawa, vyombo vya habari vya ndani viliripoti, na kuna hofu kwamba idadi ya watu waliokufa inaweza kuongezeka hadi kufikia 50. Msako wa kuwatafuta manusura unaendelea.

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk amesema ghasia hizo "za kutisha" zilionekana kuwa "matokeo ya mzozo kuhusu umiliki wa ardhi na ziwa na haki za watumiaji" na kutoa wito kwa maafisa "kuhakikisha waliohusika wanachukuliwa hatua".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live