Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FIFA kuifungia Kenya baada ya serikali kuingilia utendaji wake?

Amina Mohamed Mageuzi katika Shirikisho la Soka Kenya laitia katika hatari ya kupigwa marufuku na FIFA

Thu, 11 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kenya imejiweka katika hatari ya kufungiwa kutoka shirikisho la soka duniani Fifa baada ya Waziri wake wa Michezo kuagiza kamati ya muda kusimamia shirikisho la soka nchini humo.

Waziri wa Michezo Amina Mohamed ameunda kamati ya muda ya watu 27 kusimamia Shirikisho la Soka la Kenya (FKF).

Fifa inapinga serikali kuingilia katika uendeshaji wa mashirikisho wanachama.

"Ili kuhifadhi mchezo wa kandanda, nimeamua kuteua kamati ya walezi ya FKF kwa muda wa miezi sita," Mohamed alisema kwenye taarifa.

"Wizara ya Michezo, Utamaduni na Urithi itawezesha utendaji kazi wa kamati ya muda."

Mojawapo ya malengo yaliyotajwa ya kamati hiyo ni "kukabidhi FKF kwa maafisa wapya watakaochaguliwa baada ya uchaguzi ".

Taarifa ya Mohamed ilisema kuwa FKF "katika miaka michache iliyopita ... imekabiliwa na masuala kadhaa ya utawala ambayo yamekuwa yakisumbua sana Wizara".

"FKF imeshindwa kuwajibikia pesa zote ilizotengewa na serikali," aliandika.

Ripoti ya hivi karibuni iliyoidhinishwa na Wizara ilipendekeza kwamba mamlaka za Kenya zifanye uchunguzi zaidi ili kubaini "kiasi ambacho ufujaji wa fedha ndani ya FKF kwa lengo la kuwashtaki wale ambao wanaweza kupatikana na hatia".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live