Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ezekiel Mutua azungumza baada ya kutimuliwa KFCB

A7c6a9a7fc2ef4b8 Ezekiel Mutua azungumza baada ya kutimuliwa KFCB

Sat, 7 Aug 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Katika ujumbe wa Twitter, Jumamosi, Agosti 7, Mutua alishukuru familia yake na marafiki kwa jumbe za kutia moyo kufuatia kutimuliwa kazi kwakeKuondoka kwake KFCB kulithibitishwa na Waziri wa Mawasiliano Teknolojia (ICT), Joe Mucheru mnamo Ijumaa, Agosti 6Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mambo ya Nje (CAK), Christopher Wambua aliteuliwa na Mucehru kuchukua nafasi ya MutuaAliyekuwa Afisa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Uainishaji wa Filamu Kenya (KFCB) Ezekiel Mutua amevunja kimya chake baada ya kufutwa kazi Ijumaa, Agosti 6.

Katika ujumbe wa Twitter, Jumamosi, Agosti 7, Mutua alishukuru familia yake na marafiki kwa jumbe za kutia moyo kufuatia kutimuliwa kazi kwake.

Mutua aliongeza kusema kwamba hakuwa katika nafasi ya kujibu jumbe zote na maswali kuhusu kutimuliwa kwake afisini ghafla.

Kuondoka kwake KFCB kulithibitishwa na Waziri wa Mawasiliano Teknolojia (ICT), Joe Mucheru mnamo Ijumaa, Agosti 6.

Mucheru alisema jukumu la Mutua katika fisi ya Bodi ya Uanishaji Filamu nchini litatamatika Ijumaa, Agosti 6.

Kwa ufanisi, Waziri huyo alimteua Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mambo ya Nje (CAK), Christopher Wambua kuchukua nafasi aliyoacha Mutua. Wambua atashikilia nafasi hiyo kwa muda.

Kulingana na ripoti za Standard, CS Mucheru alikuwa ameamuru KFCB kuteua kaimu Mkurugenzi Mtendaji na kufuata utaratibu wa kumpa Mutua likizo ya lazima akisubiri kustaafu kwake Oktoba 25, 2021.

Iliripotiwa kuwa waziri huyo alimsuta Mutua na mwenyekiti wa bodi ya KFCB kwa kumuagiza Inspekta Jenerali wa Mashirika ya Serikali kuondoka wakati wa mkutano wa bodi mnamo Juni 30 ambayo ni kinyume na Sheria ya Shirika hilo la serikali.

Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) pia ilianzisha uchunguzi baada ya Mutua kushtakiwa kwa kupokea malipo na marupurupu visivyo.

Katika taarifa ya Mei 6, EACC ilisema kwamba mwanakamati wa bodi hiyo, Bi Gathoni Kungu, pia alikuwa akichunguzwa.

KFCB iliulizwa kutoa faili za kibinafsi za maafisa hao wawili, malipo yote ya mishahara na maruporupu pamoja na hati za malipo na, sera ya rasilimali watu na stakabadhi za utaratibu wa nyongeza ya mishahara na posho.



Barua ya siri aliyoandikiwa waziri Mucheru iliyopenya mitandaoni Julai 23, 2021 ilifichua mvutano uliopo katika usimamizi wa KFCB.
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke