Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ezekiel Mutua achukizwa na video chafu ya muimbaji Embarambamba

D8c132e50c213522 Ezekiel Mutua achukizwa na video chafu ya muimbaji Embarambamba

Tue, 25 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Video za Embarambamba akisakata densi na wanaume wenzake na wanawake katika hali isiyokuwa ya ustaarabu klabuni zimezua hisia mseto

- Afisa Mkuu Mtendaji wa Bodi ya Kukagua Filamu Nchini (KFCB) Ezekiel Mutua alizitazama na kusema mwanamuziki huyo alivuka mipaka na vimbwanga vyake

- Wanamtandao wengi walimuunga mkono Mutua wakiongezea kuwa lazima hatua ichukuliwe kumkabili msanii huyo wa injili

Afisa Mkuu Mtendaji wa Bodi ya Kukagua Filamu Nchini (KFCB) Ezekiel Mutua amemsuta muimbaji mcheshi Chris Embarambamba kufuatia video kumuonyesha akisakata densi katika njia isiyokuwa sawa na wanaume wenzake.

Kulingana na Mutua, mwanamuziki huyo alivuka mipaka na vimbwanga vyake.

"Embarambamba, hiyo ni mbaya.Umevuka mipaka!"aliandika Mutua kwenye Twitter.

Video za Embarambamba akisakata densi na wanaume wenzake na wanawake katika hali isiyokuwa ya ustaarabu klabuni zimezua hisia mseto.

Kutoka kwa video hiyo, muimbaji huyo anaonyeshwa akimbeba kijana huyo, akamuweka kati kati ya miguu yake na kuanza "kumpampu" kabla ya kumuweka chini na kupanda juu yake.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke