Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eymael mambo yake safi Sauzi

Eymael Pic Data Eymael mambo yake safi Sauzi

Sat, 10 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

CHIPPA United ipo kwenye hatua za mwisho za kumpa kibarua Luc Eymael ili kumrithi Dan Malesela aliyefutwa kazi kutokana na mwenendo mbaya wa timu,

Hii ni baada ya kocha huyo wa zamani Yanga SC kuruhusiwa kufanya kazi kwa mara nyingine tena nchini Afrika Kusini baada ya wanasheria wake kumpambana na kusafisha jina lake kufuatia kuhusishwa na matukio kadhaa ya kibaguzi.

Awali, Eymael aliwekewa vizuizi vya kufanya kazi nchini humo kutokana na kauli yenye viashiria vya ubaguzi wa rangi aliyotoa dhidi ya mashabiki wa Yanga, lakini kwa sasa inaelezwa kwamba kocha huyo anaweza kufanya kazi.

Awali Eymael aliwahi kufanya kazi na Black Leopards FC, Free State Stars na Polokwane City FC kabla ya kuja Tanzania kuifundisha Yanga ambayo ilimaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu Bara.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz