Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eric Omondi ampigia chapuo Mfanyabiashara Jimi Wanjigi kuwania Urais

070bcf3a44f46caf Eric Omondi ampigia chapuo Mfanyabiashara Jimi Wanjigi kuwania Urais

Fri, 3 Sep 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Mchekeshaji Eric Omondi amewataka vijana wajitokeze na wachukue uongozi wa taifa akidai kwamba Wakenya wamechoshwa na utawala wa viongozi wazee.

Kulingana na Omondi nyadhifa nyingi serikalini zimekuwa zikishikiliwa na viongozi wazee kwa zaidi ya miongo 50.

Omondi amesema taifa lilipata Uhuru miaka 57 iliyopita lakini vijana hawajatambua kuna uhuruMchekeshaji huyo alimuidhinisha Jimi Wanjigi, mfanyabiashara mkubwa nchini ambaye pia ametangaza kuwania Urais kwa tiketi ya chama cha ODM.

Kulingana na Omondi nyadhifa nyingi serikalini zimekuwa zikishikiliwa na viongozi wale wale wazee kwa zaidi ya miongo 50 na hakuna mabadiliko au maendeleo wamefanyia nchi.

Kwenye kampeni maarufu 'Fagio Wote", Omondi alisema vijana wana uwezo wa kubaini na kuchagua viongozi wanaotaka.

" Lazima tuchukuwe taifa letu, taifa hili limekuwa huru kwa miaka 57 lakini vijana hawajatambua kuna uhuru," Alisema Omondi.

Omondi aliendelea na kuwataja viongozi ambazo wamekuwa serikalini tangu nchi ilipopata uhuru na anawataka wastaafu.

" Yafaa tuwataje kwa majina, Kalonzo Musyoka, Raila Odinga, Musalia Mudavadi William Ruto, mnajijua wenyewe, wakati umefika sasa, lazima tukasirike, lazima tulichukuwe bunge, seneti na Ikulu," Aliongezea Omondi.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke