Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eric Omondi amkashifu Ezekiel Mutua kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake

0fgjhs6kd564q9id1 Eric Omondi amkashifu Ezekiel Mutua kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake

Fri, 23 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Malumbano kati ya mchekeshaji Eric Omondi na Afisa Mkuu Mtendaji wa bodi ya KFCB Ezekiel Mutua huenda yasiishe hivi karibuniOmondi amemkashifu Mutua kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake na kwa hivyo anafaa kubanduliwa afisiniMchekeshaji huyo ambaye yuko nchini Tanzania amesema akirejea Kenya atazindua kampeni ya kumtimua Mutua afisiniMchekeshaji Eric Omondi na Afisa Mkuu Mtendaji wa Bodi ya Kudhibiti Filamu Nchini KFCB Ezekiel Mutua wanaendelea kupigana vita vya maneno kuhusu sanaa na wasanii nchini.

Wawili hao wamekuwa wakitofautiana mara kwa mara kwa masuala kadhaa.

Omondi ambaye yuko Tanzania, amemkashifu Mutua kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake na amemtaka ajiuzulu badala ya kuwahangaisha wasanii.

Akiwa kwenye mahojiano na Tanzania Empire FM, Omondi ambaye anafahamika kuwa Rais wa Comedy alisema Mutua ameleta chuki kubwa kati yake naye.o

Omondi amesema akirejea nchini, atawahamasisha wasanii wenzake wambandue Mutua afisini kwa lazima iwapo hataki kuwajibika.

" Nitaanzisha kampeni ya kumtimua afisini Jumapili nitakaporejea Kenya kwa sababu ni kana kwamba ameshindwa kutekeleza majukumu yake. Nadhani pia ameamua kunichukia bila sababu, anakashifu kila kitu ninachokifanya, kiwe kizuru au kibaya," Eric alisema.

Read also

Mimi ni Mke wa Mtu Tafadhali Msipige Simu Baada ya Saa za Kazi, Chifu awaonya Wakaaji

Omondi alikamatwa hivi maajuzi kuhusiana na shoo yake ya Wife Material, iliyodaiwa kuwa chafu na kukosa maudhui.

Mchekeshaji huyo aliachiliwa huru na kisha kuamrishwa kufuta video zote alizokuwa amepakia mitandaoni na kusitisha shoo hiyo.

Wawili hao pia wamekabiliana hivi majuzi baada ya Mutua kudai kwamba wasanii ni maskini ila wengi wao wanajifanya kuwa tajiri, madai yaliowakasirisha wasanii wote.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke