Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eliud Kipchoge ang'aa kwenye mbio za Marathon nchini Uholanzi

Dd46e15e0e3bb7b2 Eliud Kipchoge ang'aa kwenye mbio za Marathon nchini Uholanzi

Sun, 18 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Kipchoge alisajili muda wa 2:04:30 kushinda mbio hizo nchini Uholanzi

- Alishinda mbio hizo miezi mitatu baada ya kupoteza taji lake kwenye mbio za London Marathon

- Mkenya Korir alikamilisha katika nafasi ya pili na muda wa 2:06:40 huku raia wa Eritrea, Goitom Kifle akimaliza udhia na muda wa 2:08:07

Eliud Kipchoge amerejea kwenye mtindo wake wa ushindi baada ya kutwaa ushindi kwenye mashindano ya NN Mission Marathon nchini Uholanzi.

Kipchoge alishinda mbio hizo miezi mitatu baada ya kupoteza taji lake kwenye mbio za London Marathon.

Wakati huo alikamilisha katika nafasi ya nane na kuwa ushinde wake wa mara ya pili kwenye mbio hizo miaka saba iliyopita.

Hata hivyo, nguli huyo mwenye miaka 35, alipiga moyo konde na kurejesha heshima yake Jumapili, Aprili 18, kwa kutwaa ushindi kwenye NN Mission Marathon iliyoandaliwa Twente Airport nchini Uholanzi.

Mbio hizo zilikuwa zimeratibiwa kuandaliwa mjini Hamburg, Ujerumani, wikendi iliyopita lakini iliahirishwa kutokana na masharti ya kuzuia kuenea kwa COVID-19.

Wakimbiaji 70 walishiriki huku bingwa wa Uholanzi Michel Butter akiwa miongoni mwao.

Raia wenzake Abdi Nageey, Bart van Numen na Frank Futselaar pia walishiriki.

Lakini Kipchoge ndiye atimaye aliibuka mshindi huku Mkenya huyo akisajili muda wa 2:04:30 kushinda mbio hizo.

Mshikilizi huyo wa rekodi ya dunia alikuwa na Wakenya wenzake Jonathan Korir na mdhibiti kasi Philemon Kacheran kwa kilomita 30 kabla ya kuongeza kasi na kutimka kukata utepe.

Hili ndilo shindano la mwisho la Kipchoge kabla ya kueleka kutetea taji lake la Olimpiki kwenye mashindano ya Tokyo 2020 ambayo yaliahirishwa hadi Agosti.

Korir alikamilisha katika nafasi ya pili na muda wa 2:06:40 huku raia wa Eritrea, Goitom Kifle akimaliza udhia na muda wa 2:08:07.

Kipchoge alisema: "Lengo langu limetimia. Hali ya hewa ilikuwa nzuri, upepo kiasi lakini sikuwa na lalama,"

"Mbio zilikuwa sawa. Hii ndio ilikuwa mtihani wa kweli kuelekea Tokyo. Ni vizuri kuwa na marathini miezi michache kabla ya Olimpiki kuniweka fit," alisema Kipchoge baada ya kutwaa ushindi.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke