Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

EABC na Marekani kuja na eneo huru la kibiashara

Afrika Mashariki EAC Baraza la Biashara Afrika Mashariki na Marekani kuja na eneo huru la kibiashara baina yao

Mon, 20 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baraza la Biashara la Afrika Mashariki EABC limesema Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zinafikiria kuanzisha mchakato wa kuandaa eneo huru la kibiashara baina yao na Nchi ya Marekani.

Hayo yamebainishwa katika Kikao baina ya Maafisa wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki EABC kilichoongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu John Kalisa pamoja na Afisa Mkuu wa Taasisi ya huduma za Biashara ya Nchini Marekani Ken Walsh kilicholenga kujadili namna bora ya kuendeleza ushirikiano wa kibiashara Baina ya Marekani na Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Katika Mazungumzo ya Kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya EABC Jijini Arusha Afisa Mkuu wa Taasisi ya huduma za Biashara ya Nchini Marekani Ken Walsh amesema mipango yao kwa sasa ni kuahakikisha wanasaidia ukuaji wa maendeleo ya Kibiashara katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika maeneo ya kilimo usafirishaji, uchukuzi na tekinolojia.

Ken Walsh amesema katika kufanikisha hilo Octoba 2022 Serikali ya Marekani itatuma ujumbe wa Wawekezaji Wakubwa kuja kutembelea Nchi za Afrika Mashariki kwa lengo la kuja kuangalia fursa za kibiashara na uwekezaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live