Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond akosa kuhudhuria sherehe ya Bathdei ya bintiye Princess Tiffah

726bba12e9065486 Diamond akosa kuhudhuria sherehe ya Bathdei ya bintiye Princess Tiffah

Sun, 8 Aug 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Diamond na Zari husaidiana kuwalea watoto wao wawili na huonyesha mfano boraMwanamuziki huyo alikuwa ahudhurie sherehe ya bathdei ya bintiye Afrika Kusinin lakini hakuweza sababu hakuwa na muda wa kutoshaKupitia kwenye mawasiliano yake na Tiffah, Diamond alimuahidi kwamba atamuandalia sherehe nono nchini Tanzania wikendi ijayoBintiye Diamond Platinumz Princess Tiffah amesherehekea miaka sita tangu kuzaliwa kwake kwenye sherehe nono iliyoandaliwa na mamake Afrika Kusini.

Diamond alikuwa ameahidi kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa ya bintiye lakini hakutimiza ahadi yake kwa ajili ya kukosa muda.

Kupitia kwenye mawasiliano yao kwenye mtandao wa Instagram, Diamond alimuahidi Tiffah kwamba atamfanyia sherehe nyingine kubwa nchini Tanzania wikendi Ijayo.

Diamond alimwambia Tiffah kwamba ameshazungumza na mamake na wanapanga jinsi watakavyosafiri nchini Tanzania kwa ajiliya sherehe hiyo.

" Nilizungumza na mama yako nikamweleza kwamba sherehe ya wa kwanza uifanyie Afrika Kusini na nyingine hapa Tanzania, nakuahidi itapamba moto sana," Alisema Diamond.

Read also

Tana River: Mama Aingia Vichakani na KSh 170k za Mahari ya Bintiye

Diamond na bintiye Tiffah huwa na uhusiano wa karibu kulingana na mawasiliano ambayo wao hukuwa nayo.

" Nakupenda sana binti yangu na lazima tuwe na sherehe nyingine hivi karibuni. Itakuwa nono kwa sababu una umaarufu hapa Tanzania," Aliongezea Diamond.

Jinsi mambo yalivyo kwa sasa, Zari na wanawe wawili huenda wakasafiri kwenda Tanzania wakati wowote.

Haya hapa baadhi ya maoni ya Wakenya;

doris_angwenyi alisema:

" Itafika mahali Diamond atahitajika kujiita mkutano na kiingereza chake na wamalize tofauti zao."

thrifting.escapades alisema:

" Hakuna mwafrika ana deni la mwingine kwa kutozungumza kiingereza safi."

elviskatana alisema:

"' Hii ni kizungu ya Super Star kweli."

francmuirur:

" Zungumza tu lugha ya mama, hakuna atakayekuuliza,"

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke