Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DRC: Mwakilishi wa serikali katika mazungumzo na M23 mjini Kampala afutwa kazi

DRC: Mwakilishi Wa Serikali Katika Mazungumzo Na M23 Mjini Kampala Afutwa Kazi .png DRC: Mwakilishi wa serikali katika mazungumzo na M23 mjini Kampala afutwa kazi

Wed, 24 Jul 2024 Chanzo: Bbc

Jean Bosco Bahala Lusheke, mkuu wa mpango wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wa kupokonya silaha na kurejesha wajeshi na waasi katika maisha ya uraia, ameondolewa kwenye wadhifa wake, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa msemaji wa Rais.

Katika ujumbe mfupi wa maandishi uliotumwa kwenye tovuti ya X na Tina Salama, msemaji wa rais Felix Tshisekedi, hakueleza sababu ya kufutwa kazi kwa Bahala Lusheke.

Mwishoni mwa wiki iliyopita iliripotiwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Bahala anaongoza timu iliyotumwa na serikali ya Kinshasa kwenda Kampala kushiriki mazungumzo ya siri na kundi la M23.

Redio ya Ufaransa (RFI) inasema imepata taarifa zilizothibitisha kuwa mazungumzo hayo yalifanyika katika hoteli ya Imperial Heights mjini Kampala, kati ya ujumbe wa serikali unaoongozwa na Jean Bosco Bahala na ujumbe wa Alliance Fleuve Congo (AFC) - muungano unaojumuisha kundi la M23 – lililowakilishwa na René Munyarugerero na Kanali John Imani.

RFI inasema wajumbe wa AFC walikubali kuwa mazungumzo haya yalifanyika, na kwamba Jean-Bosco Bahala alisema kuwa alikuwa Kampala lakini hakukutana na wajumbe wa AFC, akidai alikuwa kwenye kazi ya kawaida ya biashara na kwamba hakwenda kukutana M23.

Siku ya Jumatatu, msemaji wa serikali Patrick Muyaya alitangaza kwamba "hakuna mtu ambaye ametumwa na serikali kwa mazungumzo yoyote" na kundi la M23 "jijini Kampala".

Chanzo: Bbc