Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Corona yasababisha idadi ya ndege zinazotua Kenya kupungua

KCAAA Idadi ya ndege Kenya yaporomoka kisa UVIKO-19

Wed, 22 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kampuni binafsi ya usafiri wa anga nchini Kenya, imeuza ndege zipatazo 72 mwaka 2020 kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa UVIKO-19 uliotikisa uchumi wa nchi hiyo kwa kiasi kikubwa.

Shirika la usafiri wa anga la taifa nchini humo (KCAA) imetoa ripoti inayoonesha kupungua kwa idadi ya ndege kutoka 807 kwa mwaka 2019 hadi 735 kwa mwaka 2020, idadi ambayo wamesema ni tofauti na ndege zinazomilikiwa na Jeshi la nchini humo.

Ripoti hiyo pia imeutaja ugonjwa wa UVIKO-19 kuwa sababu kuu ya kuporomoka kwa sekta ya usafiri wa anga nchini humo kufuatia marufuku za kusafiri zilizowekwa katika mataifa karibu yote duniani.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa KCAA, Gilbert Kibe, amefafanua suala hili kwa kusema kuwa kushuka kwa idadi ya ndege nchini humo kumesababishwa na sababu nyingi lakini kubwa ikiwa ni ugonjwa huo.

"Kushuka kwa idadi ya ndege ambazo zimesajiliwa hapa nchini kuna toa tafsiri kuwa ndege hizo huenda zimeuzwa au zimeondolewa nchini kwa sababu mbalimbali lakini kubwa ni ugonjwa wa UVIKO-19" Amesema Mkurugenzi huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live