Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chiki azungumza baada ya Bien kusema yuko huru kugawa asali yake

878ae18a5e4bf31b Chiki azungumza baada ya Bien kusema yuko huru kugawa asali yake

Sun, 13 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Bien alinukuliwa akisema mkewe Chiki yuko huru kuonjesha tunda lake kwa wanaommezea mate ili kujiopa raha

- Alisema huo ndio urafiki wao katika ndoa na pia wamekwisha kufanya makubaliano hayo

- Chiki hata hivyo amewavunja moyo waliokuwa na matumaini akisema kufanya hivyo si rahisi kama wengi walivyochukulia

Chiki Kuruka amezungumza baada ya mumewe Bien Baraza kunukuliwa kwenye mazungumzo alipodaiwa kusema mkewe yuko huru kupeana tunda lake kwa wanaommezea mate.

Bien alidaiwa kusema kuwa uhusiano wao unaruhusu kila mmoja kuonja mishikaki barabarani licha ya minofu kuwa nyumbani.

Alidaiwa kusema hayo kwenye mahojiano na Sol Family ambapo walizungumzia kuhusu maisha yao kama mke na mume.

"Mimi na Chiki tumekubaliana kuwa nikikutana na msanii ambaye nammezea mate na kuwe na nafasi ya kuonja tunda, naweza kufanya hivyo. Na yeye vivyo hivyo pia," alisema Bien.



Licha ya wataalamu wa saikolojia kusema wanaume huwa ni watu wenye wivu mkubwa kufikiria wapenzi wao watapeana asali kwingine, Bien alisema yeye yuko sawa.

"Sina shida yoyote iwapo hilo ndilo anataka, ni vizuri apate atakacho. Huwezi kumfanya binadamu asifanye anachotaka. Na siwezi kupatwa na wivu, kwa sababu nataka yeye afurahie pia," alisema msanii huyo.

Chiki hata hivyo sasa amechipuka kukanusha madai kuwa anaweza kumpa dume mwingine haki ya Bien.



Alisema mali yake iko chini ya kifuli kikali na aliye na funguo za kuruhusu azuru nchi hiyo ya kutamaniwa ni Bien pekee.

Alisema kilichokuwa kikiendelea kwenye mahojiano hayo ni mzaha pekee na waliokuwa wameingiwa na matumaini kuwa wataonja tunda lake wapunguze pupa.

Mimi na Bien tulikuwa tukifanya mzaha tu pale Sol Family. Watu ndio walielewa mzaha huo vbaya. Hata hivyo, sisi huwa tuko wazi kuzungumzia matamanio yetu hata kama ni kuhusu kuwamezea wasanii fulani," alisema Chiki.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke