Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bunge la Kenya laidhinisha safari za ndege Marekani

KENYA QQQQ Bunge la Kenya laidhinisha safari za ndege Marekani

Fri, 8 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bunge la Kenya, limeidhinisha makubaliano mapya yatakayo ruhusu Shirika la ndege la KQ kuongeza wigo wa safari zake nchini Marekani kupitia mji wa New York.

Wabunge hao walipiga kura kuidhinisha utiaji saini wa makubaliano hayo ili kuruhusu Shirika la Fedha la Marekani FedEx kuanzisha kituo pamoja na shughuli za usafirishaji mizigo nchini Kenya.

Makubaliano haya yataruhusu KQ kufanya shughuli za kusafirisha abiria kutoka mji wa Nairobi hadi Mji wa New York Marekani.

Kabla ya makubaliano haya hazikuwepo safari za ndege zinazotoka Marekani kuelekea Kenya, jambo ambalo limefanya FedEx kutangaza nia ya kuanzisha kituo hicho katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta.

Kenya ilisaini makubaliano haya mapema Februali 5, 2020 yaliyorejelea mapendekezo yaliyofanyika katika mji wa Washington DC Juni 8, mwaka 2008.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live