Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bunge kuwakagua mawaziri wateule walioteuliwa na Rais Ruto

Bunge Kuwakagua Mawaziri Wateule Walioteuliwa Na Rais Ruto.png Bunge kuwakagua mawaziri wateule walioteuliwa na Rais Ruto

Tue, 23 Jul 2024 Chanzo: Bbc

Wabunge nchini Kenya Jumanne wataendelea na vikao baada ya mapumziko ya wiki tatu, kufuatia maandamano mabaya yaliyopelekea Bunge la Agosti kuvamiwa na waandamanaji tarehe 25 Juni.

Ajenda kuu ya ya bunge hilo itakuwa ni kuwakagua mawaziri 11, ambao ni sehemu ya baraza la mawaziri wateule waliotangazwa na Rais William Ruto siku ya Ijumaa wiki iliyopita.

Spika wa Bunge la taifa Moses Wetang'ula alifichua kwamba mawaziri wote wateule 11 wa Rais Ruto watafanyiwa mtihani kubaini iwapo wanafaa kushikilia nyadhifa za uwaziri zilizopendekezwa.

Baada ya shughuli za bunge kufungwa kwa ukarabati kwa takriban mwezi mmoja tangu tarehe 28 mwaka huu, linatarajiwa kurejea kwa shughuli zake huku wabunge hao wakirejea vikao vyao Jumanne kutoka mapumziko mafupi.

Chanzo: Bbc