Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bondia afariki baada ya kupigwa kwa KO ulingoni

Bondia Afariki Bondia Zimunya (kulia)

Thu, 4 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamasumbwi wa uzito wa Super bantam kutoka nchini Zimbabwe, Zimunya, 24, amefariki siku ya Jumatatu wiki hii, baada ya kuzimia wakati wa pambano lisilo la ubingwa alilopigana siku ya jumamosi ya wiki iliyopita.

Hii ni mara ya kwanza kwa bondia kufariki nchini Zimbabwe kutokana na majeraha aliyoyapata ulingoni.

Tukio hili limeleta maswali mengi, lakini Lawrence Zimbudzana, Katibu mkuu wa Bodi ya Kitaifa ya Kudhibiti Ndondi na Mieleka ya Zimbabwe (ZNBWCB), anasema kuwa mipango ya uchunguzi bado haijakamilika ili kufahamu zaidi chanzo cha kifo cha bondia huyo.

"Kwa sasa tutaangazia mazishi, na kisha tuketi na kuangalia masuala," Zimbudzana aliambia BBC Sport Africa katika mazishi ya Zimunya yaliyofanyika jana jumatano.

Taarifa iliyotolewa na ZNBWCB ilisema kuwa "taratibu zote muhimu za matibabu zilifuatwa na msaada wa dharura wa matibabu ulitolewa mahali hapo kabla ya kupelekwa hospitali".

Zimunya alipigwa makonde kadhaa kichwani katika raundi ya tatu ya pambano hilo la raundi sita.

Aliyekuwa mkufunzi wake Tatenda Gada alihuzunika, akisema nyota huyo alikuwa na uwezo mkubwa.

"Tumeondokewa na hazina kubwa ya taifa katika fani ya masumbwi," Gada amesema.

"Nilifanya kazi na Taurai kwa zaidi ya miaka minne - nilimtazama akistawi na alikuwa mmoja wa nyota wajao katika fani hii."

Baba yake Zimunya, Samson, alikuwa bondia mahiri asiye wa kulipwa na alitarajia mtoto wake angebeba jina la ukoo na kuwa bingwa.

Mashindano ya masumbwi nchini Zimbabwe yamerejea hivi karibuni baada ya vizuizi vya kupambana na janga la corona kulegezwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live