Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bilionea awa Rais Caf

6c3f7ea7ee924f1f06e74010dca43c8d Bilionea awa Rais Caf

Sat, 13 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

TAJIRI namba tisa barani Afrika, Patrice Motsepe raia wa Afrika Kusini amechaguliwa bila kupingwa kuwa Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (Caf) katika uchaguzi uliofanyika Rabat, Morocco jana.

Motsepe mwenye umri wa miaka 59 amechaguliwa kufuatia washindani wake watatu kujitoa wiki iliyopita, huku aliyekuwa Rais wa Caf tangu mwaka 2017, Ahmad Ahmad adhabu yake ya kufungiwa kujihusisha na michezo ikipunguzwa kutoka miaka mitano hadi miwili hivyo kukosa sifa ya kugombea tena.

Washindani waliojitoa wiki iliyopita ni Jacques Anouma, Ahmed Yahya na Augustin Senghor.

Akihutubia mkutano wa vyama wanachama kwenye ukumbi wa uchaguzi katika mji mkuu wa Morocco, Rabat, Motsepe alisisitiza imani yake juu ya jinsi umoja unavyoweza kutangaza enzi mpya ya mpira wa miguu wa Afrika.

Motsepe, mmiliki wa mabingwa wa Afrika 2016, Mamelodi Sundowns, moja ya timu zilizofanikiwa zaidi nchini Afrika Kusini, hapo awali alizungumzia hamu yake ya kuona timu ya Afrika ikitwaa Kombe la Dunia.

Motsepe anakadiriwa kuwa na utajiri wa Dola bilioni 3 na mwaka 2013, alikuwa mwafrika wa kwanza kutia saini ahadi ya Bill Gates na Warren Buffett, kutoa angalau nusu ya utajiri wake kwa misaada.

Chanzo: www.habarileo.co.tz