Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bilionea Afrika Kusini ilionea Afrika Kusini akaribia Urais wa Caf

Cf64a7aec2f3d3f1d09b508e73f99339 Bilionea Afrika Kusini ilionea Afrika Kusini akaribia Urais wa Caf

Mon, 8 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MMILIKI na Rais wa klabu ya Mamelod Sundown ya Afrika Kusini, Patrice Motsepe anakaribia kuunasa urais wa Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) baada ya mpinzani wake mkubwa katika nafasi hiyo, Ahmed Yahya wa Mauritania kujitoa.

Huyo ni mgombea watatu wa nafasi hiyo kutangaza kujitoa kwasababu mbalimbali tangu Ijumaa ya wiki iliyopita. Motsepe ambaye ni bilionea wa Afrika Kusini, kwa sasa ndiye mgombea pekee aliyebaki katika nafasi hiyo ya juu kabisa katika Caf.

Hata hivyo, Rais wa sasa wa Caf, Ahmad Ahmad aliyefungiwa na Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa) kujihusisha na soka kwa miaka mitano, anaweza kurejea katika kinyang’anyiro hicho endapo Mahakama ya Usuluhishi wa Mambo ya Michezo (Cas) leo itamuondolea adhabu yake.

Kama kifungo hicho cha Ahmad wa Madagasca hakitaondolewa, basi Motsepe ana kila sababu ya kuvikwa taji la urais wa Caf katika uchaguzi utakaofanyika Ijumaa.

Motsepe Mwafrika wa tisa tajiri zaidi kwa mujibu wa jarida la Forbes ambalo linakadiria kuwa na utajiri wenye thamani ya dola za Marekani bilioni 2.9. Chini ya saa 24 zilizopita, wagombea wote wanne walikuwa bado katika kinyang’anyiro hicho lakini mazungumzo yaliyofanyika Morocco wiki iliyopita walijitoa mmoja baada ya mwingine na kumuacha Motsepe pekee.

Katika taarifa yake ya kujitoa Ijumaa iliyopita, Rais wa Shirikisho la Soka la Senegal, Augustin Senghor alisema wagombea waliamua kukubali mapendekezo yaliyowasilishwa kwao na Fifa, Morocco na Misri kwa ajili ya umoja wa soka la Afrika.

Mazungumzo hayo yalitaka kila mpinzani wa Motsepe kuwasiliana na serikali yake kabla ya kuamua kujitoa, huku yule wa Ivory Coast, Jacques Anouma, Senghor na Yahya wote walitaja wakuu wao wa nchi katika taarifa zao za kujitoa.

Senghor na Yahya wanatarajiwa kujihakikishia majukumu ya umakamu wa rais, huku Anouma ambaye kama Senghor walitangaza kujitoa baadae Ijumaa. “Napenda kutangaza uamuzi niliouchukua baada ya makubaliano na wagombea wenzangu katika nafasi ya urais wa Caf, tuliamua hilo kwa ajili ya maslahi ya soka la Afrika na uamuzi huu ni wa binafsi.”

“Kwa sasa, pamoja na Patrice, Augustin na Jacques Anouma, ni wakati wa kulipa kipaumbele soka la Afrika. Haya ni makuibaliano ya kihistoria, ni maoni yangu, ni heshima kubwa kwa hatma ya Caf soka la Afrika.”

Motsepe mwenye umri wa miaka 59 amesema akichaguliwa atajenga ushirikiano na wadhamini katika sekta binafsi ili kuiongezea uwezo Caf. Kikwazo pekee kwa Motsepe kuwa kiongozi wa juu kabisa katika soka la Afrika ni kurejea kwa Ahmad katika mbio hizo.

Motsepe atakuwa Rais wa kwanza wa Caf kutoka nchi inayozungumza Kiingereza tangu kuanzishwa kwake mwaka 1957 na yenye maskani yake Cairo. Uchaguzi Mkuu wa Caf unatarajia kufanyika katika jiji kuu la Morocco la Rabat

Chanzo: www.habarileo.co.tz