Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benki za Uganda zapoteza zaidi ya Tsh bilioni 9.20 kwa udukuzi

Hacker Sc Benki za Uganda zapoteza zaidi ya Tsh bilioni 9.20 kwa udukuzi

Mon, 25 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benki za nchini Uganda zimepoteza zaidi ya dola milioni 4 sawa na shilingi bilioni 9.20 za kitanzania kwa mwaka 2020 kufutia kukithiri kwa vitendo vya udukuzi wa kimtandao.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Uganda Interpol mapema Oktoba 17, 2021.

Mkurugenzi wa kitengo hicho, Charles Birungi amesema kuwa wizi huo ulifanyika kwa kutumia teknolojia ya kibenki, kadi batili za kutolea fedha pamoja na biashara za mtandaoni.

"Katika kiwango hichi cha dola milioni 4 (Tsh bilioni 9.20), dola milioni 3 (bilioni 6.90 za kitanzania) zimetokana na matukio 10 ya wizi wa kibenki" imesema ripoti hiyo.

Licha ya kudhibiti matukio haya ya wizi nchini humo, inaelezwa kuwa juhudi hizo zingonga mwamba kila kukicha kwani wadukuzi hao wanaongeza mbinu za wizi kwa kutumia teknolojia ya juu kila mara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live