Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bei ya mafuta itashuka wiki ijayo, Raila atangaza

Mafuta Bei ya mafuta itashuka wiki ijayo, Raila atangaza

Sun, 3 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Bei ya mafuta nchini imekuwa mzigo kwa Wakenya baada ya EPRA mnamo Septemba 14 kupandisha bei ya bidhaa za mafutaBidhaa za mafuta nchini zinauzwa katika gharama ya juu ambayo Wakenya hawajawahi kushuhudia huku EPRA ikitaja kupanda kwa gharama ya uagizaji.

Raila Odinga na William Ruto ni miongoni mwa wanasiasa waliogusia suala hilo wakiomba serikali kuingilia kati na kutafuta suluhu mwafaka Suala hilo pia limefikishwa bungeni na wabunge wengi wanaonekana kukubaliana na hoja ya kupunguza bei ya mafuta lakini kinaya ni kuwa wao hao ndio walipitisha mswada wa kuongeza kwa 8% kwenye bidhaa za mafuta.

Afueni katika mjadala wa bei ya mafuta nchini, baada ya kiongozi wa ODM, Raila Odinga kudokeza kuwa serikali inatazamiwa kupunguza bei ya mafuta wiki ijayo.

Akizungumza katika kaunti ya Bungoma siku ya Jumamosi, Oktoba 2, Raila alisema hatua hiyo ni ya kuwalinda Wakenya ambao wameathirika pakubwa na ugumu wa uchumi uliosababishwa na janga la COVID-19.

"Ninawahakikishia kuwa bei ya mafuta itashuka wiki ijayo. Wakenua amabo wamekuwa awakihanagaika kuata chakua tangu mlipko wa jnga walihasikka pakubwa na kuongezeka kwa bei ya mafyta," alisema.

Matamashi ya Raila yanakujia baada ya Mamlaka ya Kusimamia Kawi na Petroli Nchini (EPRA) mnamo Septemba 14, kupandisha bei ya bidhaa za mafuta.

EPRA ilishtumiwa vikali baada ya kutangaza kuwa bei ya mafuta itapanda.

Bei hiyo mpya ilishuhudia petroli, dizeli na mafuta taa zikiongezwa kwa KSh 7.58, KSh7.94, na KSh 12.97 kila lita mtawalia.

Hivyo petroli, dizeli na mafuta zinauzwa KSh 134.72, KSh 115.60, na KSh 110.82 kila lita mtawaliwa jijini Nairobi, ikiwa ni gharama ghali zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini.

Katika taarifa tofauti, TUKO.co.ke iliripotia kuwa Uhuru aliagiza bei ya umeme kupunguzwa kwa 33% katika kipindi cha miezi minne zijazo.

Hii ni baada ya Uhuru kupokea ripoti ya Jopo la Rais kuhusu Makubaliano ya Ununuzi wa Umme nchini.

Jopo hilo lililobuniwa Machi 2021, lilikabidhiwa mamlaka ya kusahisisha sheria za umeme na kurekebisha makubaliano ambayo ilitiwa saini na KPLC.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke