Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bandari Kuu Sudan yakalia kuti kavu

Port Sudan Bandari Kuu Sudan yakalia kuti kavu

Mon, 18 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bandari kuu ya Sudan, ambayo imegawanyika katika vituo sita maalum pamoja na soko kuu la maonesho ya kibiashara , imekuwa ikipitia vikwazo vingi vya kibiashara kwa zaidi ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwake kipindi cha ukoloni.

Wafanyabiashara pamoja na kampuni zinazofanya shughuli zake katika bandari hiyo wamelazimika kuhamishia safari za meli kubwa za mizigo kutoka katika banari hiyo hadi nchi jirani kufuatia kukithiri kwa mshambulizi ya waandamanaji wanaoishinikiza Serikali ifunge bandari hiyo.

Tayari meli kubwa nyingi zimehama na kuanza kuhusha kontena katika bandari ya Ain Al Sokhna ya nchini Misri ambayo inasifika kwa kuwa na mazingira rafiki ya kibiashara pamoja na kodi nafuu kulinganisha na bandari ya Sudan.

Wafanyabiashara wengine hasa kutoka Mashariki mwa Asia wanaojihusiha na biashara za magari a vifaa vya magari wametimkia Benghazi na Libya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live