Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Babangida afunga ndoa na wake wawili kwa siku moja

Mme 660x400 Babangida afunga ndoa na wake wawili kwa siku moja

Thu, 11 Mar 2021 Chanzo: millardayo.com

Kiongozi wa chama cha vijana All Progressives Congress (APC) Mjini Abuja nchini Nigeria, Babangida Sadiq amefunga ndoa na wake zake wawili kwa siku moja huku akidai ametimiza ndoto zake ambazo alikuwa anatamani kufanya hivyo tangu alivyokuwa mtoto.

Harusi zake zote zimefanyika siku ya Jumamosi Machi 6 mjini Abuja, na wake zake wamefahamika kwa majina ya Maryam Muhammad na Maimuna Mahmud, harusi ya kwanza imefanyika saa 4 Asubuhi nyingine imefanyika 7 Mchana.

Akizungumzia sababu ya kuoa wake wawili baada ya kufunga ndoa Babangida Sadiq amesema “Kwa muda mrefu ndoto zangu ilikuwa kuoa wanawake wawili kwa siku moja, watu wengi wanahisi haiwezekani lakini Mungu amefanya nimefanikisha hili” .

EXCLUSIVE: MAAJABU YA MTOTO GENIUS WA HESABU, “SIJAFUNDISHWA, WAKUBWA HAWANIWEZI”

Chanzo: millardayo.com