Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amunike amkumbuka Magufuli

Pic Amunike Data Amunike amkumbuka Magufuli

Sat, 20 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

ALIYEWAHI kuwa kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike ameshindwa kujizuia juu ya msiba wa Rais John Pombe Magufuli.

Amunike alikiongoza kikosi cha Stars kilichofuzu Afcon 2019 baada ya kuichapa Uganda 3-0 mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Baada ya Stars kufuzu, Magufuli aliwapa viwanja wachezaji wote waliokuwa katika timu hiyo, huku pia akimzawadia kiwanja bondia Hassan Mwakinyo aliyetoka kumpiga bondia wa Argentina, Sergio Gonzalez.

Akizungumza na Mwanaspoti akiwa nyumbani kwake nchini Hispania, Amunike alisema: “Natoa pole kwa familia yake (Rais Magufuli)pamoja na Watanzania kwa ujumla, mmepoteza mmoja wa viongozi bora waliowahi kutokea barani Afrika.”

Kwa upande wa aliyewahi kuwa kocha wa Mwadui FC, Ally Bizimungu akizungumzia msiba huyo, alisema: “Magufuli hata mimi mwenyewe ameniumiza sana, kumpata mtu kama yeye itachukua muda sana, Mungu amuwekee wepesi na mapumziko mema.”

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz