Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajitoa kwenye tuzo baada ya mashabiki kumpinga mitandaoni

Artist Mwanamuziki wa Zambia, Slapdee

Wed, 13 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki maarufu kutoka Zambia, Mwila Musonda maarufu kama "Slapdee" amejiondoa kuwania tuzo baada ya mashabiki kumkosoa kwa kupafomu katika kampeni za chama tawala cha Patriotic Front katika uchaguzi uliofanyika miezi michache iliyopita.

Chama kilichokuwa madarakani, Patriotic Front kilishindwa uchaguzi na hivyo kuondoka madarakani mwezi Agosti.

Slapdee, awali alitetea maamuzi yake ya kufanya maonesho kwa ajili ya waogombea wa chama hicho kama biashara lakini inaoneka iliathiri muziki wake.

Kufuatiwa kuchaguliwa kushiriki kuwania tuzo za Afrimma, Wazambia walihamasisha watu mitandaoni kumpigia kura mwanamuziki wa Afrika Kusini Cassper Nyovest katika kipengele alichokuwa anawania cha Mwanamuziki bora wa kiume kusini mwa Afrika ambapo kulikuwa na mshiriki wa Zimbabwe Jah Prayzah, Tha Dogg kutoka Namibia na wengine wengi.

Kampeni za kumpinga Slapdee, na kumuunga mkono Cassper Nyovest zilizua gumzo mtandaoni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live