Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika Kusini yajiondoa kwenye shindano la Miss Universe Israel

Asdghf.png Afrika Kusini yajiondoa kwenye shindano la Miss Universe Israel

Mon, 15 Nov 2021 Chanzo: BBC

Serikali ya Afrika Kusini imejiondoa katika ufadhili wa Miss Afrika Kusini katika shindano la Miss Universe litakalofanyika Israel.

Kumekua na wito wa kumshinikiza Bi Lalela Mswane kususia mashindano hayo hayo licha ya waandalizi kusema kuwa haifai kuingizwa siasa.

TWale wanaopinga kushiriki wa Afrika Kusini katika mashindano hayo wanalalamikia madai kwamba Israel ilitekeleza ukatili dhidi ya Wapalestina.

Waafrika Kusini wanasema wanafahamu fika siasa za ubaguzi wa rangi hivyo basi hawaungi mkono kile kinachoendelea nchini Israel.

Katika tarifa, Wizara ya sanaa na utamaduni nchini Afrika Kusini imesema kuwa "ukatili uliofanywa na Israel dhidi ya Wapalestina umenakiliwa vyema" na haukuweza "kwa dhamiri njema kujihusisha na vile".

Israel hapo awali ilikanusha kufanya ukatili na inakataa shutuma kwamba vitendo vyake dhidi ya Wapalestina ni sawa na ubaguzi wa rangi.

Waziri Nathi Mthethwa ameelezea kwamba kujiondoa kwa Bi Mswane kungeweza kuwa mzuri kwa hadhi ya kimataifa ya Afrika Kusini "ikilinganishwa na tukio la mara moja ambalo linaweza kuwa mbaya kwa mustakabali wake na hadhi yake ya umma kama mwanamke kijana, mweusi".

"Jambo hili halijafanikiwa, hivyo basi uamuzi wa kuitenga hadharani kwa serikali na watu wa Afrika Kusini na msimamo wa mratibu wa shindano la Miss SA kuhusu suala hili", alisema.

Shindano la Miss Universe limepangwa kufanyika tarehe 12 Desemba.

Chanzo: BBC