Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika Kusini kuandaa Kombe la Dunia la Vilabu

SAFA President Danny Jordaan Rais wa Shirikisho la Soka Afrika Kusini, Danny Jordaan

Tue, 14 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Shirikisho la Soka Afrika ya Kusini, Danny Jordaan amesema nchi yake ina nia ya kuwa mwenyeji Mashindano ya dunia kwa upande wa vilabu itakapofika Disemba mwaka huu baada ya nchi ya Japan kujitoa kutokana na Janga la COVID-19.

Jordaan ameliambia Shirika la Associated Press, atakutana na Katibu Mkuu wa FIFA, Fatma Samoura katika Mji wa Lagos, Nigeria wiki hii kujua ni vitu gani vya msingi wanahitajika kuviwasilisha kwa mamlaka hiyo ili kupata kibali cha kuandaa Mashindano hayo.

Mashindano ya Dunia kwa upande wa vilabu yatahusisha bingwa wa Ulaya, klabu ya Chelsea na washindi wa mabara mengine, aidha mshindi wa Ligi kuu katika nchi inayoandaa Mashindano pia anapata nafasi.

"Shirikisho la Soka lazima lipate kibali kutoka kwa Serikali kuandaa mashindano, hivyo vikao na Waziri wa Michezo pia tumeshapanga" amesema Jordaan. "Tutajua nafasi yetu mwishoni mwa wiki hii" amesema

FIFA ilitangaza wiki iliyopita kuwa,Japan imejitoa katika kuandaa Mashindano hayo kama nchi mwenyeji kwa sababu ya hofu ya kulipuka kwa maambukizi mapya baada ya kumalizika kwa mashindano ya Olimpiki kwa watu wenye Ulemavu.

Afrika ya Kusini ina viwanja mbali mbali ambavyo vilijengwa na kukarabatiwa kwa ajili ya Michuano ya Kombe la Dunia lakini dhamira yake hiyo itategemea na kiwango na mwenendo wa hali ya Virusi vya Corona nchini humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live