Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AS Vita: Hatuiogopi Simba

F2d29e7a6a4f3cc33e2e53acfb3edf7d AS Vita: Hatuiogopi Simba

Mon, 29 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KOCHA Mkuu wa AS Vita ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Florent Ibenge amesema hawaiogopi Simba bali wanaiheshimu hivyo wana uwezo wa kuifunga nyumbani.

Timu hizo zinatarajiwa kukutana mwishoni mwa wiki hii katika mechi ya makundi kweye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mechi hiyo imepangwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili jana, Ibenge alisema wanafahamu uzuri wa Simba, lakini hawaiogopi na watapambana kupata ushindi.

Katika mechi ya kwanza iliyofanyika Kinshasa, DRC, AS Vita ililala kwa bao 1-0.

“Tunajua Simba inacheza vipi ikiwa nyumbani na tunafahamu kwa kiasi gani wanahitaji ushindi na sisi pia tunataka kusonga mbele hivyo ni lazima tutafute ushindi,” alisema Ibenge.

Vita haipo vizuri sana msimu huu kwenye michuano hiyo baada ya kufikisha pointi nne ikishinda dhidi ya Al Merrikh 4-1 ugenini na kutoka sare ya 2-2 na mabingwa Al Ahly ugenini lakini ilifungwa 3-0 nyumbani Kinshasa na timu hiyo ya Misri.

Hata hivyo, timu hiyo imeonekana kufanya vizuri ikiwa ugenini msimu huu kuliko nyumbani, jambo ambalo Simba inabidi ijipange kucheza nayo.

Simba inaongoza kundi A ikiwa na pointi 10 ikihitaji pointi mmoja kufuzu robo fainali ya michuano hiyo. Al Ahly iko nafasi ya pili ikiwa na pointi saba na AS Vita ni ya tatu ikiwa na pointi nne.

Vita ikishinda itafikisha pointi saba na hivyo kufufua matumaini ya kusonga mbele.

Timu mbili za juu ndizo zinazofuzu hatua ya robo fainali. Simba iliwahi kufika hatua hiyo msimu wa mwaka 2018/19.

Chanzo: www.habarileo.co.tz